Saturday, August 31, 2013

Waendesha piki piki maarufu kama boda boda wachapwa viboko

Waendesha pikipiki kwa jina maarufu la boda boda wamemuomba waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dr. Emmanuel Nchimbi kusikiliza kilio chao kutokana na baadhi wa askari wa usalama barabari kuwachapa viboko wanapokamatwa kwa makosa mbali mbali.

wengine walifika mbali zaidi na kudiriki kusema ni bora warudi kwenye uhalifu kuliko kuendelea na kazi hii.Pamoja na kuchapwa viboko lakini pia wamekuwa wakiombwa rushwa.


No comments: