Friday, September 13, 2013

Jamaa mmoja atiwa luango Mbeya kwa kuwasumbua zima moto wamsaidie kujiunga na Freemason

Propaganda za kuhusu Freemason ambazo zimeendelea kushika kasi siku hadi siku katika jamii yetu zimefanya baadhi ya watu waendelee kuacha kufanya shughuli za kimaendeleo ambazo zinaweza kuwaingizia kipato bali wamekuwa wakiwaza jinsi ya kupata hela za haraka haraka kutokana na kitu kiitwacho Freemason.

Siku hizi imekuwa kitu cha kawaida kabisa kuona matangazo mbalimbali yamebandikwa mitaani kuwa kuna mganga anaweza kukusaidia kujiunga na freemasom kwa kiasi cha fedha kuanzia laki moja.

Jamaa mmoja huko jijini Mbeya alijikuta akitiwa mbaroni baada ya kuwa mara kwa mara akipiga simu idara ya zima moto simu namba 114 ili waweze kumsaidia kujiunga na freemason, jamaa huyo alikuwa amedanganywa na wenzie kuwa idara ya zima moto ni idara ya freemason, na yeye kwa kutokulielewa hilo na kutaka utajiri wa haraka haraka akaanza kuwasumbua idara hiyo ya zima moto ili waweze kumsaidia, mara kwa mara amekuwa akipiga simu na kuambiwa kuwa idara hiyo haiusiki na mambo hayo hakuamini akawa anaendelea kusumbua.  Baada ya kuona usumbufu, wafanyakazi hao wa idara hiyo ya zima moto wakaamua kumuwekea mtego na kumwambia kuwa ni kweli idara hiyo ilikuwa inahusika na swala hilo hilo walipanga wakutane sehemu ili waweze kumkabidhi pesa hizo za freemason.

Jamaa bila ajizi akakubaliana nao na walipokutana ndipo walipomkamata na kumpeleka polisi.

Wito umeendelea kutolewa kuwa watu waache kupenda pesa za haraka haraka badala yake wafanye kazi kwa bidii na waachane na masuala ya freemason, pia watu waache kudanganya wenzao hasa wa huko kijijini kuhusu mambo yasiyokuwa na msingi.

No comments: