Sunday, September 29, 2013

Majambazi yavamia benki ya I & M na kupora kiasi kikubwa cha fedha

Majambazi ambayo idadi yao ilikuwa saba yalivamia benki ya I & M ya jijini Dar es salaam iliyokuwa mtaa wa Indira Ghandi eneo la Posta jijini Dar es Salaam  siku ya Jumamosi tarehe 28/9/2013  majira ya saa tatu na nusu asubuhi na kupora kiasi kikubwa cha fedha kinachofikia shilingi milioni mia moja na hamsini.  MMoja wa majambazi hao alikuwa amevalia sare za polisi. Kutokana na tukio hilo kamanda wa kanda maalum Suleiman Kova ameagiza kuwekwa kwa askari wenye silaha kwenye benki zote nchini.


No comments: