Saturday, October 12, 2013

Kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru 2013 mkoani Iringa

Kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2013 zinatarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Iringa katika viwanja vya Samora siku ya Jumatatu tarehe 14 October 2013, kilele hicho kinaenda sambamba na kumbukumbu ya miaka kumi na nne ya kifo cha Mwalimu Nyerere. Sherehe hizo zitatanguliwa na misa ya kumuombea baba wa  Taifa ambayo itafanyika katika kanisa Katoliki Kihesa.  Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.  Kauli mbiu mwaka huu ni watanzania ni wamoja, tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasillimani.

No comments: