Friday, October 11, 2013

P-Square kufanya onyesho moja jijini Dar es Salaam

Wanamuziki wa kundi la P-square Peter na Paul Okoye ambao ni mapacha, wanatarajia kufanya onyesho moja la muziki tarehe 23 mwezi Novemba jijini Dar es Salaam ambalo litakuwa la live band, hayo yalisemwa jana Alhamisi tarehe 10/10/2013 na mtangazaji wa kipindi cha Uswazi Zembelwa wakati akiongea katika kipindi cha Hot Mix kinachorushwa hewani kila siku za Ijumaa kuanzia saa 11 jioni katika luninga ya E ATV. Onyesho hilo linaratibiwa na EATV pamoja na EA radio.  Mdhamini wa onyesho hilo ni Vodacom (T).  P-Square wanatarajia kuwasili na wanamuziki kumi na tatu ingawa pia atasindikizwa na wanamuziki wa nyumbani ambao watatangazwa baadaye.  Malengo ya onyesho hilo ni kuleta 
burudani.




No comments: