Tuesday, October 1, 2013

Mvua yaleta madhara Dar es Salaam

Mvua iliyonyesha jijini Dar Es Salaam jana tarehe 30/9/2013 imeleta madhara makubwa sana katika baadhi ya maeneo hasa maeneo ya Buguruni. Baadhi ya nyumba zilikuwa zimezingirwa na maji hata kupelekea maji kufikia watu vifuani ambao walikuwa wanajaribu kuokoa vyombo vyao visiweze kuchukuliwa na maji.  Katika baadhi ya maeneo masofa yalionekana yakielea kwenye maji.  Waathirika wamesema vitu vingi vimesombwa na maji mfano pesa, unga, mchele, nguo za shule za watoto.  

Tatizo kubwa linalosababisha adha hizi kwa wananchi mara kwa mara pindi mvua zinaponyesha ni miundo mbinu mibovu, pia watu wengi wamejenga kuta ambazo kuwa zinazuia maji kupita pindi mvua inaponyesha.






No comments: