Sunday, October 13, 2013

Umoja wa Africa umeazimia hakuna kiongozi yeyote wa Africa aliye madarakani atashtakiwa na mahakama ya ICC

Azimio hilo limechukuliwa katika kikao chao kilichofanyika hivi karibuni mjini Addis Ababa Ethiopia. Viongozi hao wamechukua hatua hiyo kutokana na kile kinachoonekana kuwa mahakama hiyo inawalenga viongozi wa Africa zaidi kuliko viongozi toka bara lingine, wametoa mfano kuwa kati ya mwaka 2004 hadi sasa kuna kesi 30 katika mahakama ya ICC kati ya hizo 27 zinawahusu viongozi wa nchi za Africa. Kutokana na maazimio hayo Rais Uhuru Kenyatta hatohudhuria kesi inayomkabili katika mahakama ya kimataifa ya ICC hadi hapo atakapomaliza muda wake wa uongozi.


No comments: