Wednesday, October 2, 2013

Maduka yote jijini Mbeya yafungwa kupinga ununuzi wa mashine za TRA

Vurugu zimezuka leo jijini Mbeya leo  maeneo ya Mwanjelwa wakati wafanyabiashara walipopinga kununua mashine za TRA ambazo kila moja zinauzwa kiasi cha shilingi laki nane.

Maduka yote yalionekana yamefungwa.  Kwenye baadhi ya sehemu yalionekana magurudumu ambayo yamechomwa moto kuzuia magari kupita.


Kuna baadhi ya sehemu magari yalikuwa yamepangwa barabarabi.
Maduka haya yaliyopo Mwanjelwa yote yalifungwa kupinga ununuzi wa mashine hizo za TRA.


No comments: