Wednesday, October 9, 2013

Mzee Majuto kugombea ubunge 2015

Msanii wa sanaa za vichekesho 'King Majuto' ambaye jina lake halisi ni  Amri Athumani  ametangaza nia yake ya kugombea ubunge katika jimbo la Tanga mjini kwa chama cha Mapinduzi ifikapo 2015 Mwenyezi Mungu akimpa uhai.
King Majuto  mwenye umri  zaidi ya miaka 60 ametangaza nia yake hiyo alipohojiwa na Clouds FM katika kipindi cha amplifier siku ya Jumatatu kinachorushwa hewani kila siku za Jumatatu na Ijumaa kuanzia saa 1 jioni hadi saa 3 za usiku.



No comments: