Saturday, October 12, 2013

Walemavu wa familia moja wanahitaji msaada wa hali na mali

Watoto watano kati ya nane wa familia moja wenye huko Chome Same wanahitaji masaada wa hali na mali ili waweze kuendesha maisha yao kutokana na  ulemavu wa viungo walionao.  Kutokana na maelezo ya mama mzazi Nirenjigwa Joseph watoto hao walizaliwa wazima ila walipata ulemavu baada ya kuanza kutembea. Baba wa watoto hao Amini Joseph Amini  alifariki  mwaka 1992  baada ya hapo yeye  amekuwa akilelea familia hiyo.

Watoto hao Joseph  Amini ( 38), Nafikahedi ( 33) ,Wediel (30) Gadison (28) na Julius (25) wote ni walemavu wa viungo ambao hutembea kwa kutambaa. Wanahitaji kuwa na mwangalizi wakati wote kwa hakuna wanaloweza kufanya bila usaidizi,

Kwa sasa ukiwaangalia watoto hao tayari wameshakuwa wakubwa kabisa na changamoto kubwa ni kwamba familia haiwezi kuwaacha kukaa pekee yao kwani wapo pia wa kike.Baada ya kutembelea familia hiyo waliona kuwa jamii hiyo inahitaji kusaidiwa kwani wanapoishi walemavu hao hakuna kivuli. Pia, wamekuwa wakitambaa kwenye jua na kusumbuliwa na tatizo la funza hivyo watasaidia kuweka baraza kwenye nyumba hiyo. Wamesema wataendelea kuhamasisha na jamii ili iisaidie familia hii.
Kwa mtu yeyote atakayeguswa kuweza kuisaidia familia hii anaweza kuwasiliana na Chediel Amini ambaye amebeba jukumu la kuwasaidia ndugu zake kwa simu namba 0654118385.




No comments: