Sunday, October 13, 2013

Mwandishi wa Habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amelazwa katika kitengo cha wagonjwa wa dharura katika hospitali ya taifa Muhimbili

Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi amewaambiwa waandishi wa habari waliopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili kuwa mwandishi wa ITV na Radio One Ufoo Saro amelazwa katika kitengo cha wagonjwa wa dharura katika hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupigwa risasi mapema leo.  Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam Hemed Msangi amesema Ufoo Saro amepata majeraha tumboni na begani, upelelezi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

No comments: